Habari za dunia kwa Kiswahili

DW KISWAHILI

 • 15 November 2019: Watu 420,000 wapoteza makaazi kufuatia mafuriko Sudan Kusini - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Shirika la kimataifa la misaada la Save the Children limesema zaidi ya watu 420,000 wamelazimika kuondoka kwenye makaazi yao kutokana na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko Sudan Kusini.
 • 15 November 2019: Ujerumani yawatuliza raia wake baada ya IS kurejea nchini humo - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Serikali kuu ya Ujerumani inajaribu kuwatuliza wananchi kuwa usalama wao hautoingia hatarini kwa kurejea humu nchini wafuasi wa kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislam-IS kutoka Uturuki.
 • 15 November 2019: Maandamano yazidi kuutikisa mji wa Hong Kong - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza katika mitaa ya Hong Kong huku uharibifu mkubwa ukishuhudiwa jimboni humo. Maandamano hayo yanaendelea licha ya onyo la rais wa China Xi Jinping.
 • 15 November 2019: Kenya na Somalia zakubaliana kurekebisha mahusiano - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Kenya na Somalia zimekubaliana kurekebisha mahusiano yao na kuanza tena kutoa vibali vya kusafiri kwa raia wao baada ya msuguano wa muda mrefu kuhusu mpaka wa baharini ambao ulitia doa uhusiano wa mataifa hayo jirani.
 • 15 November 2019: Wafanyakazi wa shrika la ndege la Afrika Kusini wagoma - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Wafanyakazi wa shirika la ndege la Afrika Kusini SAA wameanza mgomo juu ya viwango vya mishahara na kupunguzwa kwa nafasi za kazi katika hatua iliyolilazimisha shirika hilo kufuta karibu safari zake zote za ndege.

BBC SWAHILI

IPS SWAHILI