Habari za dunia kwa Kiswahili

DW KISWAHILI

 • 20 October 2017: Viongozi EU waidhinisha mazungumzo ya maandalizi Brexit - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuanza mazungumzo ya maandalizi kuhusu uhusiano wa kanda hiyo na Uingereza baada ya Brexit, licha ya kusisitiza kwamba hakuna hatua muhimu zilizopigwa katika mazungumzo.
 • 20 October 2017: Kenyatta aonya wanaotaka kuleta vurugu - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Rais Uhuru Kenyatta amewahakikishia usalama Wakenya watakaopiga kura katika uchaguzi mpya siku ya Oktoba 26. Amesema serikali yake iko tayari kupambana na tishio lolote la usalama wa taifa wakati na baada ya uchaguzi.
 • 20 October 2017: Weinstein alitaka kulala na Lupita Nyong'o - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Mwigizaji huyo mashuhuri kutoka Kenya anaeleza jinsi ambavyo Harvey Weinstein, meneja ya kampuni ya utengenezaji filamu, alimnyanyasa kijinsia. Weinstein anasakatwa na sakata la unyanyasaji wa wanawake kadhaa.
 • 20 October 2017: Shinikizo laongezeka kwa viongozi wa jimbo la Catalonia - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Serikali ya Uhispania inajiandaa kutwaa mamlaka ya ndani ya utawala wa jimbo la Catalonia. Serikali hiyo kuu imepata uungwaji mkono kutoka kwa upinzani wa kulivunja bunge la Catalonia na pia kuandaa uchaguzi mpya.
 • 20 October 2017: Mazungumzo kuunda serikali ya Muungano Ujerumani yaanza - DW-WORLD´s Kiswahili Homepage
  Duru ya kwanza ya mazungumzo rasmi yatakayofanikisha kuundwa kwa serikali ya muungano, itakayokuwa ya kwanza kuhusisha pande nne, inaanza leo.

BBC SWAHILI

IPS SWAHILI